Thursday, 5 January 2017

KINANA AWASILI ZANZIBAR KUZINDUA KAMPENI ZA CCM LEO



https://www.facebook.com/boniphace.nyabweta?fref=ts

KINANA AWASILI ZANZIBAR KUZINDUA KAMPENI ZA CCM LEO



Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (watano kulia) na ujumbe wake wa viongozi waandamizi kutoka makao makuu ya CCM, wakiwa kwenye chumba cha nahodha walipokuwa wakisafiri kwa boti ya mwendokasi kutoka Dar es Salaam, kwenda Zanzibar kwa ajili ya kushiriki uzinduzi wa kampeni za CCM, uchaguzi mdogo wa ubunge jimbo la Dimani, leo. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rodrick Mpogolo
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akihoji moja ya kifaa cha kuongozea boti ya mwendo kasi kinavyofanya kazi.
Karibu Zanzibar
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Rodrick Mpogolo akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mjini Magharibi, Aziza Mapuri baada ya msafara wa Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana kuwasili Bandari ya Zanzibar leo
"NAAM TUMEWASILI KWA MUDA SAHIHI" Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akimwambia Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Zanzibar Vuai Ali Vuai baada ya kuwasili Bandari ya Zanzibar leo
Katibu Mwenezi wa CCM, Humphrey Polepole (kushoto) baada ya kuwasili Bandari ya Zanzibar
Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara Rodrick Mpogolo (kushoto) alipowasili Bandari ya Zanzibar leo
Humphrey Polepole akilakiwa baada ya msafara wa Kinana kuwasili Afisi Kuu ya CCM, Kisiwandui leo
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mjini Magharibi Aziza Mapiri akitoa maelezo kwa Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana kuhusu hali ya kampeni za uchaguzi mdogo wa Ubunge jimbo la Dimani  walipokuwa katika Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar leo
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana na msafara wake wakitazama eneo alilouliwa muasisi wa Mapinduzi ya zanzibar, Hayati Abeid Amani Karume katika Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar, leo
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiagwa na viongozi wakati akitoka Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar kwenda kwenye mapumziko kabla ya kwenda kwenye uzinduzi wa kampeni za uchaguzi mdogo jimbo la Dimani leo jioni. (Picha zote na Bashir Nkoromo)
TANGAZO

0 comments:

Post a Comment