TRUMP AWAFUTA KAZI MABALOZI WOTE WANAOWAKILISHA MAREKANI DUNIANI
Rais
wa Marekani Donald Trump amewafuta kazi mabalozi wote wa nchi hiyo kote
duniani na wanaohudumu katika mashirika ya kimataifa.
Kwa mujibu wa taarifa ya mtandao wa Independent, mabalozi hao wametakiwa kuachia nafasi zao mara moja na kurudi nyumbani.
Kiongozi
huyo juzi alifanya ziara yake ya kwanza katika ofisi za makao makuu ya
shirika la Ujasusi la Marekani CIA, na kuvituhumu baadhi ya vyombo vya
habari nchini humo wakati akitoa hotuba yake, kwamba vinawagawa
wananchi.
Zaidi
ya mabalozi 80 wa Marekani katika nchi mbali mbali duniani walifutwa
kazi Ijumaa tarehe 20 Disemba saa sita mchana punde baada ya Trump
kuapishwa.
Hatua
hiyo ya Trump inatazamiwa kuvuruga uhusiano na wa itifaki muhimu kama
vile Ujerumani, Uingereza, Canada. Inatabiriwa kuwa nchi hizo zinaweza
kukaa bila mabalozi kwa miezi kadhaa kwani baada ya Trump kuteua
mabalozi wapya watalazimika kuidhinishwa na Bunge la Kongresi kabla ya
kuanza kazi zao.
Source: Independent
TANGAZO



0 comments:
Post a Comment