RAIS DKT MAGUFULI AFANYA MAZUNGUMZO NA RAIS WA UTURUKI, WAHUTUBIA MKUTANO WA WAWEKEZAJI NA WAFANYABIASHARA WA NCHI ZAO
Rais
wa Jamhuri ya Uturuki Mhe Recep Tayyip Erdogan na mkewe wakipokea
mashada ya maua kutoka kwa watoto walipowasili Ikulu jijini Dar es
salaam leo Januari 23, 2017 kwa mapokezi rasmi na mazungumzo na
mwenyeji wao Rais Dkt John Pombe Magufuli.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na mkewe
Mama Janeth Magufuli wakiwalaki Rais wa Jamhuri ya Uturuki Mhe Recep
Tayyip Erdogan na mkewe Emine Erdogan walipowasili Ikulu jijini Dar es
salaam leo Januari 23, 2017 kwa mazungumzo.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na mgeni
wake Rais wa Jamhuri ya Uturuki Mhe Recep Tayyip Erdogan wakipiga ngoma
Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 23, 2017
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na mkewe
Mama Janeth Magufuli wakiwazawadia Kinyago cha Umoja na Mchoro wa Mlima
Kilimanjaro Rais wa Jamhuri ya Uturuki Mhe Recep Tayyip Erdogan na mkewe
Emine Erdogan walipowasili Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 23,
2017
Mke
wa Rais Mama Janeth Magufuli na mke Rais wa Jamhuri ya Uturuki Mama
Emine Erdogan wakipeana mikono baada ya maongezi Ikulu jijini Dar es
salaam leo Januari 23, 2017.
Rais
wa Jamhuri ya Uturuki Mhe Recep Tayyip Erdogan akiongea baada ya yeye
na mwenyeji wake Rais Dkt Magufuli ushuhudia uwekaji saini mikataba
mbalimbali ya ushirikiano kati ya serikali ya Tanzania na Uturuki Ikulu
jijini Dar es salaam leo Januari 23, 2017
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na akiongea
katika kongamano la wawekezaji wa Tanzania na Uturuki katika ukumbi wa
BoT jijini Dar es salaam leo Januari 23, 2017
Rais
wa Jamhuri ya Uturuki Mhe Recep Tayyip Erdogan akiongea katika
kongamano la wawekezaji wa Tanzania na Uturuki katika ukumbi wa BoT
jijini Dar es salaam leo Januari 23, 2017.
Rais
wa Jamhuri ya Uturuki Mhe Recep Tayyip Erdogan akiongea na mwenyeji
wake Rais Dkt John Pombe Magufuli katika kongamano la wawekezaji wa
Tanzania na Uturuki katika ukumbi wa BoT jijini Dar es salaam leo
Januari 23, 2017.
Rais
wa Jamhuri ya Uturuki Mhe Recep Tayyip Erdogan na mwenyeji wake Rais
Dkt John Pombe Magufuli wakishuhudia ubadilishanaji hati baada ya
kusaini baina ya mwenyekiti wa Wafanyabiashara wa sekta binafsi Dkt
Reginald Mengi na kiongozi wa msafara wa wafanyabiashara wa Uturuki
katika kongamano la wawekezaji wa Tanzania na Uturuki katika ukumbi wa
BoT jijini Dar es salaam leo Januari 23, 2017.
PICHA NA IKULU
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli
akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya mazungumzo na mgeni
wake Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan (kulia) Ikulu leo jijini Dar
es Salaam.
Rais
wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan akizungumza na waandishi wa habari mara
baada ya mazungumzo na mwenyeji wake Rais Dkt. John Pombe Joseph
Magufuli (hayupo pichani) Ikulu leo jijini Dar es Salaam.
Rais
wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan akikagua gwaride mara baada ya
kupokelewa na mwenyeji wake Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli (hayupo
pichani) Ikulu jijini Dar es Salaam leo.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan
akiteta jambo na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Majali (katikati) na Katibu
Mkuu Kiongozi Mhandisi Balozi John Kijazi.
Baadhi
ya viongozi wa Serikali ya Jamhuri ya Miuungano wa Tanzania (waliokaa
upande wa kulia) wakiweka saini katika mikataba na wawakilishi kutoka
Serikali ya Uturuki leo jijini Dar es Salaam. Jumla ya mikataba tisa
imetiwa saini, ikiwemo ushirikiano wa kimaendeleo.
Waziri
wa Fedha na Mipango wa Serikali ya Tanzania akibadilishana hati ya
makubaliano na Waziri wa Fedha wa Uturuki leo jijini Dar es Salaam.
UT5b:
Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) Dkt. Ayoub Ryoba
akibadilishana hati ya makubaliano na mwakilishi wa Serikali ya Uturuki
leo jijini Dar es Salaam.
Rais
wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan akiwapungia mkono wakazi wa jiji la Dar
es Salaam waliofika kumlaki katika viwanja vya Ikulu leo.Kushoto kwake
ni Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli.
Baadhi
ya wananchi wakimlaki Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan alipowasili
katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam leo. Rais huyo yupo nchini
kwa ziara ya kikazi ya siku moja ambapo katika ziara hiyo Tanzania na
Uturuki wameingia makubaliano katika mikataba tisa kwa lengo la
kushirikiana na kusaidiana.
Baadhi
ya wageni walioambatana na Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan
wakiingia katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam leo.
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye akiteta jambo
na Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Harrison Mwakyembe walipokuta wakati
wa ugeni wa Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan( hayupo pichani) leo
jijini Dar es Salaam.
Rais
Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiwa ndani ya gari na mgeni wake Rais
wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan mara baada ya kumaliza mazungumzo Ikulu
jijini la Dar es Salaam leo.
Rais
Dkt. John Pombe Joseph Maguli na mgeni wake Rais wa Uturuki Recep
Tayyip Erdogan (walioshikana mikono) wakiwa katika picha ya pamoja na
baadhi ya Mawaziri na viongozi kutoka Serikali za Tanzania na Uturuki
leo jijini Dar es Salaam.
(Picha na Frank Shija – MAELEZO)
TANGAZO














0 comments:
Post a Comment