MAKUSANYO YA KODI KIPINDI CHA NUSU MWAKA WA FEDHA 2016/17
Katika
kipindi cha miezi sita ya mwaka wa Fedha 2016/17 yaani kuanzia Julai
hadi Disemba 2016, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imekusanya kodi
jumla ya shilingi trilioni 7.27 ikilinganishwa na shilingi trilioni 6.44 ambazo zilikusanywa kipindi kama hicho mwaka wa fedha 2015/16.
Ukusanyaji wa mapato katika kipindi cha nusu mwaka wa fedha 2016/17 umeongezeka kwa asilimia 12.74. Mlinganisho wa makusanyo ya mapato kwa mwaka wa fedha 2015/16 na 2016/17 ni kama ifuatavyo:
MWEZI
|
MWAKA 2015/16
|
MWAKA 2016/17
|
Ongezeko
|
JULAI
|
925,384.7
|
1,069,458.5
|
15.57
|
AGOSTI
|
923,316.9
|
1,154.222.5
|
25.01
|
SEPTEMBA
|
1,132,310.3
|
1,378,048.9
|
21.70
|
OKTOBA
|
1,037,179.8
|
1,131,094.9
|
9.05
|
NOVEMBA
|
1,027, 939.6
|
1,123,509.7
|
9.30
|
DISEMBA
|
1,403, 189.8
|
1,414,921.8
|
0.84
|
JUMLA
|
6,449,321.1
|
7,271,256.26
|
12.74
|
Jitihada
mbalimbali zinafanywa ili kuhakikisha TRA inaongeza makusanyo kwa
kuongeza ufanisi katika ukusanyaji, kuhimiza maadili mema kwa watumishi,
kuboresha mifumo ya ukusanyaji, kushirikiana na vyombo vingine vya dola
na wananchi katika kuziba mianya ya upotevu wa mapato pamoja na
kufuatili, kuhimiza matumizi ya mashine za kielektronik na kuhimiza
ulipaji wa kodi ya majengo.
TRA
inaendelea kuhimiza wafanyabiashara wote waliosajiliwa na Kodi ya
Ongezeko la Thamani (VAT) kuwasilisha ritani za VAT kabla ya tarehe 20
ya kila mwezi kama ilivyobadilishwa katika Sheria ya Fedha ya 2016.
Pamoja
na hayo tunawakumbusha na kuwahimiza wananchi wa Dar es Salaam ambao
hawajafanya uhakiki wa taarifa za Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi
(TIN) kuhakiki taarifa zao kabla ya tarehe 31 Januari 2017 ili zoezi
hilo liweze kuanzishwa katika mikoa mingine.
TRA
inatoa wito kwa wafanyabiashara kulipa kodi stahiki kwa hiari na wakati
ili serikali ipate mapato yake ambayo yataiwezesha kuwahudumia wananchi
wake kikamilifu.
Kwa
wafanyabiashara wenye madeni ya nyuma wanashauriwa kujitokeza kuonana
na Mameneja wa Mikoa na Wilaya kujadiliana jinsi watakavyolipa madeni
yao bila kuathiri biashara zao.
Wamiliki wa majengo wanaaswa kutoa ushirikiano kwa kulipia ankara zao za kodi ya majengo kwa hiari.
‘Pamoja Tunajenga Taifa Letu’
Richard M. Kayombo
MKURUGENZI WA HUDUMA NA ELIMU KWA MLIPAKODI
TANGAZO



0 comments:
Post a Comment