MTANZANIA ALIYENGARA MASHINDANO YA KUPIKA DUNIANI AREJEA NCHINI
Mshindi wa nne wa mashindano ya mapishi duniani, Fred Uisso akionesha tuzo yake aliyokabidhiwa hivi karibuni katika fainali za mashindano hayo nchini Marekani baada ya kuwasili jana uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam leo.
Chef Fred Uisso akiwa na mkewe Monica Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa wa Bodi ya Utalii Tanzania( TTB), Geofrey Tengeneza waliofika kumpokea Mpishi huyo kutoka Mgahawa wa Africando aliyeipeperusha vyema bendera ya taifa.
Nifuraha ya kurejea na ushindi...
Tuzo aliyopewa Uisso baada ya kuibuka akiwa nafasi ya nne kati ya washiriki 458 kutoka mataifa mbalimbali huku kutoka Afrika akiwa peke yake.
Chef Fred Uisso akimkabidhi Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa wa Bodi ya Utalii Tanzania( TTB), Geofrey Tengeneza, bendera ya taifa pamoja na Tuzo hiyo baada ya kumpokea uwanja wa ndege leo.
TANGAZO
0 comments:
Post a Comment