TANZANIA KUANZA KUTUMIA MFUMO WA DIRISHA MOJA LA HUDUMA (ELECTRONIC SINGLE WINDOW SYSTEM)
Kaimu Kamishna Mkuu TRA, Mary Maganga.Katika
kuhakikisha inaboresha huduma kwa wafanyabiashara ambao wanaingiza
mizigo nchini kwa njia ya bandari, mipaka na viwanja vya ndege, Serikali
kupitia Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) imeeleza mpango wa Serikali wa
kuanza kutumia mfumo wa Dirisha Moja la Huduma (Electronic Single Window
System) ambao kwa hakika utamaliza tatizo la mizigo kukaa muda mrefu
kwa sababu ya kukosekana vibali.Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumalizika mafunzo ya siku moja kuhusu mfumo wa Dirisha Moja la Huduma kwa taasisi zinazotoa vibali na wafanyabiashara, Meneja Mfumo wa Kieletroniki wa Dirisha Moja la Huduma, Tinka Felix alisema lengo la kuanza kutumia mfumo huo ni kuboresha huduma ambazo wanazitumia sasa ili wafanyabiashara wanaoingiza mizigo nchini waweze kuipata kwa haraka kuliko ilivyo sasa.
Meneja
Mfumo wa Kieletroniki wa Dirisha Moja la Huduma, Tinka Felix
akizungumza kuhusu mfumo wa Dirisha Moja la Huduma (Electronic Single
Window System). (Picha zote na Rabi Hume - MO DEWJI BLOG)Alisema Tanzania haitakuwa nchi ya kwanza kutumia mfumo huo na mataifa mengi yanautumia ili kurahisisha huduma kutolewa kwa haraka kwani mfumo wa sasa wa forodha (tancis system) unashindwa kufanya kazi kwa haraka jambo ambalo linasababisha mizigo kuchelewa kutolewa kutokana na muda mrefu mmiliki kutumia kutafuta vibali.
Mkurugenzi
wa Sera Utafiti Na Ushauri wa TPSF, Gili Teri akizungumza faida za
kutumia mfumo wa Dirisha Moja la Huduma (Electronic Single Window
System).Alisema kwa sasa kuna taasisi za Serikali 47 ambazo zinatoa vibali lakini mfumo wa Dirisha Moja la Huduma utatumiwa na taasisi 32 ambazo kwa pamoja zitakuwa zikitoa vibali 106.
Aidha alisema Serikali imeagiza kuwa mfumo huo uanze kutumika baada ya mwaka mmoja hivyo wanategemea kuanzia mwakani mfumo ambao watakuwa wakitumia utakuwa ni wa Dirisha Moja la Huduma (Electronic Single Window System) ambao utawezesha wafanyabiashara ambao wanatoa mizigo kupitia bandari, mipaka au viwanja vya ndege kupata vibali kwa haraka.
Na Rabi Hume, MO DEWJI BLOG
Baadhi
ya washiriki wa semina hiyo ya siku moja wakiuliza maswali na kutoa
maoni kuhusu mfumo wa Dirisha Moja la Huduma (Electronic Single Window
System).

, UTAMADUNI AFRIKA MASHARIKI NA KATI
TANGAZO


0 comments:
Post a Comment