MATUMIZI YA BIOTEKNOLOJIA YA KISASA KATIKA KILIMO NI UKOMBOZI KWA WAKULIMA NA TAIFA KWA UJUMLA
Watafiti wakiwa lango kuu la kuingia katika shamba
la jaribio la mahindi yaliyoboreshwa kwa kutumia Teknolojia ya uhandisi
jeni (GMO), chini ya mradi wa Wema katika Kituo cha Utafiti wa Kilimo
cha Makutupora mjini Dodoma. Watafiti hao walikuwa wameongoza na Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Charles Tizeba kutembelea shamba hilo.
Mshauri wa
Jukwaa la Bioteknolojia Tanzania (OFAM), Dk. Nicholaus Nyange (kulia),
akitoa mada ya matumizi ya Bioteknolojia ya kisasa katika sekta ya
kilimo mbele ya Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Charles Tizeba mjini
Dodoma.
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech), Dk.Hassan Mshinda (kulia), akitoa maelezo mbele ya Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Charles Tizeba (wa pili kushoto), alipotembelea
shamba la jaribio la mahindi yaliyoboreshwa kwa kutumia Teknolojia ya
uhandisi jeni (GMO) lililo chini ya mradi wa Wema katika Kituo cha
Utafiti wa Kilimo cha Makutupora mjini Dodoma juzi.
Msafara ukielekea kwenye shamba hilo la majaribio.
Waziri Tizeba (wa sita kutoka
kushoto), akiwa katika picha ya pamoja na watafiti wa kilimo mbele ya
shamba hilo la majaribio ya mbegu za mahindi katika kituo cha kilimo cha
Makutupora mkoani Dodoma.
Watafiti na Waziri Tizeba wakijadiliana mbele ya shamba hilo.
Na Dotto Mwaibale, Dodoma
MATUMIZI ya Bioteknolojia ya Kisasa katika Sekta ya Kilimo nchini yataleta mafanikio makubwa kwa wakulima na taifa kwa ujumla.
Hayo yalielezwa na Mshauri wa Jukwaa
la Bioteknolojia Tanzania (OFAM), Dk. Nicholaus Nyange wakati akitoa
taarifa kwa Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Charles Tizeba
alipotembelea shamba la jaribio la mahindi yaliyoboreshwa kwa kutumia
Teknolojia ya uhandisi jeni chini ya mradi wa Wema katika Kituo cha
Utafiti wa Kilimo cha Makutupora mjini Dodoma.
"Matumizi ya Bioteknolojia kwa
Maendeleo ya Kilimo Tanzania ni muhimu hasa katika kipindi hiki ambacho
maeneo mengi ya nchi yanakabiliwa na ukame kutokana na tabia nchi"
alisema Dk.Nyange.
Alisema taaluma ya uhandisi jeni
inawezesha kuhamisha jeni kutoka kwa kiumbe hai kimoja na kuingiza
katika kiumbe hai kingine ili kupata sifa lengwa na kutengeneza bidhaa
kwa matumizi mbalimbali.
Akizungumzia kuhusu usalama wa
matumizi ya Bioteknolojia hapa nchini alisema ni vema kuanza mchakato wa
kuendeleza mazao yaliyofanyiwa mabadiliko ya kijenetiki (GMO) ambayo
yameleta mafanikio makubwa katika nchi nyingine kwa mfano mahindi
yanayostahimili ukame na bungua muhogo unaostahimili ugonjwa wa batobato
na michirizi kahawia, migomba yenye ukinzani dhidi ya ugonjwa wa
mnyauko na pamba yenye ukinzani kwa wadudu waharibifu.
Dk. Nyange alisema Changamoto kubwa
iliyopo katika matumizi ya teknolojia hiyo ni kuongezeka kwa upotoshaji
kutoka kwa wanaharakati na wapinzani kutokana na
ufahamu na uelewa wa watafiti,
viongozi, wanasiasa na umma kwa jumla kuhusu masuala ya taaluma hiyo
kuwa bado ni mdogo ukiwemo uwekezaji mdogo katika utafiti na maendeleo.
(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)
TANGAZO







0 comments:
Post a Comment