KESI YA MAUAJI YA WAFANYABIASHARA WA MADINI NA DEREVA TEKSI ; CHRISTOPHER BAGENI WAKUHUKUMIWA KUNYONGWA HADI KUFA ZOMBE NA WENZAKE WAACHIWA HURU
Aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi wa Wilaya ya Ilala Christopher Bageni amehukumiwa kunyongwa hadi kufa baada ya Mahakama ya Rufani Tanzania kutengua hukumu iliyomwachia huru na kumtia hatiani kwa kosa la mauaji ya wafanyabiashara wa madini watatu na dereva teksi mmoja.
Kadhalika mahakama hiyo imewaachia huru Mkuu wa Upelelezi wa zamani (wakati huo Mkoa wa Dar es Salaam) (RCO), Kamishna Msaidizi wa Polisi mstaafu Abdallah Zombe na wenzake wawili baada ya ushahidi wa rufaa hiyo kushindwa kuwatia hatiani.
Mara baada ya hukumu kusomwa, ghafla Bageni aliduwaa wakati wenzake wakimkumbatia huku wakibubujikwa na machozi wakiwa kizimbani.
“Namshukuru Mungu...Lakini nasikitika kwa Bageni kukutwa na hatia sina raha kabisa....” alisema ASP Makele wakati akitoka katika ukumbi namba moja wa mahakama hiyo.
Akizungumza baada ya hukumu hiyo, ACP mstaafu Zombe alisema anamshukuru Mungu na kuhusu Bageni alisema hana cha kuzungumzia.
Msajili alisema awali Mahakama Kuu iliyoketi chini ya Jaji Salum Massati (wakati huo kabla ya kupanda kuwa jaji wa rufani), ilimuona Zombe na wenzake hawana hatia na kwamba haiwezi kuwahukumu kwa kosa la kusaidia kufanyika mauaji hayo.
Alisema Mahakama ya Rufani inakubaliana na Jaji Massati kwamba mtuhumiwa hawezi kutiwa hatiani bila kuthibitisha mtu aliyetenda kosa hajashtakiwa na kutiwa hatiani.
TANGAZO


0 comments:
Post a Comment